Chimbuko, Maenezi Na Ukuaji Wa Kiswahili (Introduction to Kiswahili Literature and Ethnology)

Course Unit Title

Chimbuko, Maenezi Na Ukuaji Wa Kiswahili (Introduction to Kiswahili Literature and Ethnology)

Side Navigation

Course Unit Description

Kiini cha kozi hii ni kumwezesha mkufunzi kutambua na kujua mwanzo au chibuko la lugha ya Kiswahili, maenezi, ukuaji, sijili, matamshi bora na matumizi ya mapambo ya lugha kama vile vitendawili, methali, misemo na nahau.  Aidha, itamfanya mkufunzi kujuvunia lugha ya Kiswahili na kushiriki katika ukuaji wa lugha kwa kuzingatia maswala ibuka K. V. siasa, ukimwi, utandawazi na teknolojia pamoja na uvumbuzi wa kisayansi.

Malengo (Aims)

Lengo la kozi hii ni kumwezesha mkufunzi:

  • Kueleza umuhimu wa lugha huku akizingatia sajili mbalimbali za lugha.
  • Kutega na kutegua vitendawili.
  • Kuongea kwa matamshi bora na mapambo ya lugha K. V. methali, misemo na nahau.
  • Kutambua nafasi ya simulizi za hadithi na nyimbo/mashairi katika kuwipamba lugha.
  • Kuelezea historia fupi ya Kiswahili.
  • Kujieleza kwa njia ya kuwavutia wasikilizaji.

Shabaha (Learning Outcomes)
Mwishoni mwa kozi mkufunzi ataweza:

  • Kuelezea umuhimu wa lugha fasaha na yenye maadili.
  • Kuelezea historia ya Kiswahili K. V. chimbuko, maenezi, ukuaji na sajili mbali mbali.
  • Kutilia makazo lahaja za usanifishaji wa Kiswahili.
  • Kuzitamka irabu, konsonanti, na herufi mwambata ipasavyo.
  • Kutega na kutegua vitendawili.
  • Kutambua na kutumia hadithi, methali, nyimbo, mashairi, misemo na nahau katika lugha.